JP Magufuli: Nataka niwe kama Mzee Kikwete

Dk. John Pombe Magufuli, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema anataka kukaa Ikulu kwa miaka 10 kama Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ili akamilishe miradi aliyoanzisha na bdo inaendelea.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Sept. 2020, wakati akiomba kura wananchi wa Kishapu mkoani Shinyanga, akiwa njiani kuelekea Mara kuendelea na kampeni zake za urais.

Magufuli ameomba apewe tena miaka mitano ili aonyeshe dunia itakavyokwenda.

“Amekuja Mzee Kikwete mmepima kwa miaka 10, mimi miaka mitano ndio maana nawaomba mnipe tena miaka mitano, tuone dunia itakavyokwenda,” amesema Dk. Magufuli.

Amesema, katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake, ameleta maendeleo licha ya kwamba baadhi ya watu wanabeza utendaji wake.



Tunaingia awamu ya pili ya uchumi, hakuna alietegemea pale Maswa kuwe na viwanda vya chaki, hapa Muwena barabara ya lami nzuri na wanapita watu wa vyama vyote.

“Hata wanaotukana wanapita hapa hapa, shukrani ya punda ni mateke lakini sisi wajibu wetu nikufanya kazi kwa ajili ya Watanzania wote,” amesema Rais Magufuli.

Dk. Magufuli amewaomba wana CCM na Watanzania kwa ujumla kumchagua kwa kuwa, maendeleo hayana chama.

“Ndio maana nawaomba wana CCM wenzangu na wa vyama vingine mtupe kura, sababu maendeleo hayana chama,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

Vitu 5 Wanaume Wanataka Kutoka Kwa Wanawake Kwa Siri Lakini Wanaogopa Kuomba

Maji Ni Uhai kunywa maji kwa wingi utapata manufaa haya:

JE WAJUA NINI MATUMIZI YA SHANGA AU CHENI ZA KIUNONI WAKATI WA TENDO LA NDOA?!