Maji Ni Uhai kunywa maji kwa wingi utapata manufaa haya:
Asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji. Kwa hivyo, ili mwili kufanya kazi vizuri ni lazima uwe na maji ya kutosha. Unywaji wa maji una faida nyingi na kwanza husaidia mwili katika kudumisha usawa wa umajimaji wa mwili. Kazi ya maji ya mwilini ni, ufyonzaji, usambazaji, utengenezaji wa mate, usafirishaji wa virutubisho, na udumishaji wa joto la mwilini.
Kuna faida nyingi zinazopatikana katika kunywa maji kila siku
Hapa ni faida kuu za unywaji maji.
1. Matatizo ya choo Maji ni dawa ya kutibu ukosefu wa choo, kunywa maji ya kutosha kila siku na utajiepusha na tatizo la ukosefu wa choo mara kwa mara.
2. Usafishaji wa mwili Maji husaidia katika kuondoa sumu mwilini kwa kutoa uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa.
3. Kupunguza uzito Unywaji wa maji mengi unasaidia kupunguza uzito, kwani maji hayana mafuta, kalori wala sukari.
4. Tiba ya kichwa kuuma Dalili ya mtu kupungukiwa maji mwilini ni kuumwa kichwa. Unashauriwa kunywa maji ya kutosha na hautasumbuliwa sana na kuumwa kichwa mara kwa mara.
5. Nishati ya mwili Mwili unapopungukiwa maji, hukufanya ujihisi mchovu, hivyo kwa kunywa maji ya kutosha kila siku utakuwa mwenye nguvu. Pendelea kunywa maji badala ya vinywaji baridi mfano soda, juisi au bia. Habari Nyingine: Mvulana mdogo mwenye ujuzi wa kunengua awasha moto mtandaoni
6. Ngozi nyororo Unywaji maji ya kutosha kila siku unaweza kuisafisha ngozi yako na kuifanya ionekane nyororo na ya kupendeza.
7. Afya ya moyo Unywaji wa maji ya kutosha unaweza kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo. Utafiti uliofanywa Marekani kwa muda wa miaka sita umeonesha kuwa watu wanaokunywa glasi za maji zisizopungua 5 kila siku, hujiepusha na uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo kwa asilimia 41 zaidi ya wale wanaokunywa glasi 2 au chini ya hapo.
8. Usafishaji wa mwili Maji husaidia kuondoa sumu mwilini kwa kutoa uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa.
9. Mazoezi Mwili unapokuwa na maji ya kutosha, yatakufanya uwe na nguvu ya kufanya mazoezi yako ya kutosha, hivyo kupata hivyo kupata faida ya mazoezi ipasavyo.
10.Utajiepusha na saratani ya tumbo kwa kunywa maji, kwani maji husaidia suala la usagaji wa chakula tumboni na hivyo wakati wote tumbo lako litakuwa safi. Utajiondoa katika hatari ya kupata saratani ya tumbo kwa asilimia 45 na asilimia 50 kwa saratani ya kibofu cha mkojo.
11.Tiba kwa magonjwa ya zinaa haswa UTI
*Haijawai tokea mtu akaenda kumuona dakatari alafu baada ya tiba asiambiwe Kunywa Maji Mengi, Maji ni uhai tunyweni maji kwa wingi ata Ray alivyoulizwa mbona unazidi kuwa mweupe alijibu Anakunywa Maji Mengi
Comments
Post a Comment