Lissu Amjibu JPM Kazi Ndogo Ndogo
LISSU: MWAMBIENI KAZI NDOGO NDOGO ANAWAPA ALIOWAOKOTA MAJALALANI NA WANAJIJUA
-
Kufuatia kauli ya mgombea wa Urais kupitia CCM, John Pombe Joseph Magufuli ya kuwaambia wananchi wa Singida wamshauri mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema, Tundu Antiphas Lissu ajitoe kwenye uchaguzi na yeye atampatia kazi ndogo ndogo Serikalini, Lissu alitoa majibu yafuatayo wakati anaongea na wananchi wa Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha;
1.”Wanaopenda vikazi vidogo vidogo ni wale wanaookotwa jalalani.”
2.”Ikiwa ananipenda kama alivyodai alipokuwa kwetu Ikungi na asimame aseme ni akina nani walinipiga risasi 16 kwenye majengo ya Serikali yake?”
3.”Kwakuwa ananipenda na aseme kwanini alikataza serikali yake isinitibu nilipopigwa risasi 16?”
4.”Kwa kuwa ananipenda na aseme ni nani alikusudia auawe kwa kile alichosema anamsumbua sumbua kwenye masuala ya madini siku alipokuwa anapokea ripoti ya makinikia.”
5.”Baada ya Oktoba 28 mwaka huu hatakuwa na nafasi ya kumpa mtu kazi kwani atakuwa anafungasha virago kuelekea kwao Chato kwa kuwa ndiye atakuwa Rais wa kwanza kuongoza Tanzania kwa awamu moja ya miaka mitano.”

Comments
Post a Comment