Vitu 5 Wanaume Wanataka Kutoka Kwa Wanawake Kwa Siri Lakini Wanaogopa Kuomba
Wanaogopa kuongea kwa hofu ya kukataliwa au kuonekana kama wanaume wako na umama.
Yafuatayo ni Miongoni mwa mambo ambayo wanapenda kutoka kwa wanawake lakini wanaogopa kusema:
1.Kushikwa Na Kubanwa
Wanaume wanataka kushikiliwa karibu na kubanwa. Kama vile wanawake wanavyojiamini wanaposhikiliwa vizuri, wanaume hujivunia na hufurahiya sana harakati hizo. Wanataka kushikwa mikono au mabega haswa wanapotembea katika sehemu zenye watu wengi. Inawafanya wahisi salama na kwao wanaamini ni ishara ya kuonya mtu yeyote anayetamani mpeni wake.Wengi wanasema "Wanaume ni kama watoto"
2 Kukumbatiwa hadharani
Wakati wako na kikundi cha wanaume wenzao au mahali pa umma, wanaume wanataka kila mtu ajue ni nani mwenza wao anayewajali. Watakubali salamu lakini kwa siri wanataka kukumbatiwa. kitu cha kujivunia.
3 Kutumiwa ujumbe mfupi
Upendo haupaswi kuonyeshwa kwa njia moja pekee bali pande zote.Imezoeleka kwamba kwa asilimia kubwa wanaume ndo huanna kutuma meseji na akika kimya basi hakutakua na kuchati. Wanaume wanapenda jumbe nuri za asubuhi na usiku mwema. Inawapa kiburi na ujasiri wa kuendelea kupenda zaidi. Pia wanataka kutumiwa meseji kwanza kwao ili kuhisi mtu anawajali sana.
4 Kuthaminiwa
Wanataka kutambuliwa. Wanataka kutengewa. Wanataka mtu atoe maoni juu ya mitindo yao. Wanahisi kuthaminiwa wakati jambo dogo linaonekana kutoka kwao.
5 Kuitwa Majina Kupendezesha Nafsi
Nani alisema kuwa wanawake tu wanapaswa kuitwa majina matamu na ya kupendeza? Wanaume pia wanataka kuhisi kupendwa na moja ni kwa kuitwa majina matamu ya kupendeza kama boo, babe, honey,hubby,dear... na mengineyo ..Jina kama hilo linawahamasisha na ni uthibitisho kwamba mtu anahisi haswa jinsi wanahisi kwao.
Wanawake kama ukitaka kumfurahisha mpenzi wako mfanyie haya na utaona matokeo.
Comments
Post a Comment